HEADER

HEADER

Wednesday, August 13, 2014

RUMAFRICA ILIVYO WEZA KUSEMA MACHACHE JUU YA UJIO WA VIDEO YA ANGEL BENARD YA "NEED YOU TO REIGN" NCHINI KENYA

Mwanadada Angel Benard sasa amekuja kivingine kabisa kuanzia uimbaji hadi video zake. Mungu anazidi kumuonyesha njia iliyo sahihi katika kazi yake ya kumtuminkia. Angel mara nyingi amekuwa akilia sana na waimbaji wenzake kuwa wanatakiwa kufanya vitu vikali vya kumtukuza Mungu. Tumebweteka sana katika kazi ya Mungu, tunaichukulia simple sana, waswahili wanasema "Bora liende" Tunatakiwa kuwa na hamu ya kufanya vizuri kwa utukufu wa Mungu.

Angel Beanrd akiwa location

Leo hii mdada wa Yesu amekuja kuonyesha mfano na changamoto kwa waimbaji wengine kutafuta watu wenye kiwango katika v0ideo zao ili ziwe na viwango vya kimataifa na ikiwezekana kazi za walokole ziwe mfano mkubwa kwa watu wa mataifa. Tukumbuke tunamtumikia Mungu ambaye ni tajiri sana, lakini kazi zetu zinaonekana zimechoka sana. Tuache kupenda vitu vya bei chini bali tuangalie thamani ya huyu tunayemtumikia

Angel Benard ambaye mara nyingi huonekana akiwa na furaha na amani anapofanya kazi ya Mungu, kama unavyomuona

Hongera sana Angel Benard kwa hatu uliyofikia mpaka ukaamua kuvuka boda mpaka nchini Kenya kufanya kazi na watu wenye uwezo mkubwa. Hujaogopa mapesa meni bali umeangalia kile Mungu ameweka ndani yako. Mungu atafanya jambo kwa kupitia nyimbo zako hizi kali ambazo hazibagui ni mtuwa dini gani wa kusikiliza.

Angel Beanrd akitafakari jambo katika zoezi la kuandaa video yake
Angel Benard akiongea na Rumafrica kwa njia ya Watsap amesema kazi yake ya kideo hiki inafanywa na director Kevin Bosco na imefanyiwa katika mazingira ya Old Stonange Paradise Nairobi Kenya na wimbo ni "Need you to reign"

SIKILIZA NYIMBO MPYA AMBAZO ZINAFANYIWA SHOOTING HIVI KARIBUNI ZA ANGEL BENARD. SUBTITLE IMEFANYWA NA RUMAFRICA









No comments:

Post a Comment