HEADER

HEADER

Monday, June 30, 2014

MAPICHA: MUNGU NI MWEMA KWANGU DAIMA

Ninalindwa, ninatunzwa, ninalishwa, ninavishwa na huyu mpenzi wa roho yangu YESU KRISTO. Sitomwacha kamwe na ninamuomba asiniache kamwe maisha mwangu. Yesu amekuwa mfariji wangu ninapopitia magumu, hakika ni faraja yangu.

 Mungu amenipa kazi ya kumimbia, nami ninafanya kama alivyoniambia.
 Yesu Kristo hunipa kicheko kila kuitwapo leo
 Ninaringa kwasababu ninaye Yesu Kristo, naye ananipenda sana...
 Upendo na marafiki zangu ni moja ya amri ya Yesu Kristo ambayo ninajitahihidi kutekeleza

 Unaonaje ukimpenda huyu Yesu Kristo maisha mwako
Najua unapitia magumu lakini yupo mwokozi wa hayo yote ambaye ni Bwana Yesu Kristo. Mkubali sasa

Thursday, June 26, 2014

MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI WAAGWA JIJINI DAR LEO


SISTA Cresensia Kapuli aliyepigwa risasi Jumatatu Juni 23, 2014 maeneo ya Ubungo, River Side na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hatimaye ameagwa katika Parokia ya Makoka, Kibangu jijini Dar.

Mwili wa marehemu umeagwa na umati wa watu wa rika zote wakiwemo viongozi wa dini na serikali. Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Juni 28, 2014. Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!


Masista wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Sista Cresensia Kapuli aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Juni 23, 2014.


Sista Brigitte Mbaga aliyekuwa na marehemu Cresensia Kapuli eneo la tukio siku alipopigwa risasi akiwa na simanzi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond H. Mushi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick.

Mwakilishi wa mama watawa wakuu wa shirika la malkia kutoka Mbeya akilia kwa uchungu.


Jeneza likiwekwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Mbeya kwa maziko.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KUUNGANA NA KANISA LA TAG KUSHEREKEA MIAKA 75 YA UHAI MKOANI MBEYA -ASKOFU MKUU WA TAG DKT. BARNABAS MTOKAMBALI

Rumafrica ilifika katika Makao Makuu ya Kanisa la TAG Ubungo hapa jinni Dar es Salaam na iliweza kuhudhuria kikao kilichoandaliwa na Askofu Mkuu Dk. Barnabas Mtokambali  ambapo aliweza kutueleza juu ya sherehe ya miaka 75 ya uhai wa kanisa la TAG itakayofanyia mkoani Mbeya katika viwanja vya Sokoine siku ya tarehe 13/07/2014. Mkutano huu ulihudhuriwa na waandishi wa habari mbalimbali.  Askofu Mkuu Dk. Barnabas alikuwa na haya ya kusema:
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali
Ninawasalimu nyote katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, karibuni hapa TAG Makao Makuu.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) linasherekea miaka 75 ya uhai  wake hapa nchini, tangu lilipoanzishwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu mwaka 1939. Kwa kuzingatia umuhimu wa maadhimisho hayo, Mkutano Mkuu wa TAG, (chombo cha kimaamuzi) katika kikao chake cha kwanza mwaka 2012, uliamua kutangaza mwaka 2014 kuwa ni wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 ya TAG

Kutokana na maadhimisho hayo, kanisa la liliandaa maadhimisho katika ngazi zake mbalimbali za kimaongozi, kuanzia kanisa la mahali pamoja, sehemu (section) majimbo ambayo ni sawa na mikoa ya kikanisa na ngazi ya taifa ambayo kilele chake ni Julai 13 mwaka huu, katika uwanja wa sokoine Mbeya na Raisi wa Jamhuri wa Muungano Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, atakuwa  Mgeni Rasmi.

Katika maadhimisho hayo yatakayokusanya watu zaidi ya 2,000, mjini Mbeya, pia atakuwepo mwenyekiti wa makanisa ya Assemblies of God Duniani, Dk. George Wood, Maaskofu kutoka mataifa mbalimbali kama vile; Amerika, Uingereza, Ethiopia, Zambia, Rwanda, Malawi, Msumbuji, India na wengine wengi.

Wakati huu wa kuadhmisha miaka 75 ya kanisa letu, ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa yale aliyotuwezesha kufanya kwaajili ya kuujenga Ufalme Wake na kudhihirisha upendo wetu kwa jamii kwa kushiriki katika masuala mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji mkubwa.

Wakati wa maafa kama njaa, mafuriko na majanga mengine ya kijamii kwa neema ya Mungu kanisa la TAG limejihusisha kikamilifu kusaidia kwa kugawa vyakula katika mikoa ya Dodoma na kwingine, pia limechimba visima katika maeneo yenye ukame.

Mwaka huu wa maadhimisho kanisa la TAG limekuwa na miradi mingi iliyoelekeza waumini wake katika kuchangia damu mahospitalini karibu kila wilaya nchini, wagonjwa wameongezwa damu zilizotoka kwa wenzao wa TAG wakiongozwa na viongozi wa kitaifa. Pia kanisa la TAG limepeleka misaada ya kimwili na kiroho kwa waliofungwa gerezani, vituo vya yatima na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika kilele cha maadhimisho ya kanisa letu kule Mbeya, kanisa limeamua kutoa vyandarua zaidi ya 35,000 vyenye thamani zaidi ya Tsh. 270 milion. Vyandarua hivi vitagawiwa kwa kila kitanda cha hospitali katika mikoa ya Nyanda za Juuu Kusini, mikoa ya Njome, Mbeya na Rukwa, bila kujali hospitali husika inamilikiwa na nani.

Lengo la kugwa vyandarua hivi ni kuhakikisha kuwa ugonjwa wa malaria ambao kwa miaka mingi umeongeza kwa kusababisha vifo, hasa vya watoto na wajawazito unakabiliwa ipasavyo.

Pamoja na misaada hii ya  moja kwa moja, kanisa la TAG lipo katoika mcjhakato makini wa kusaidia Watanzania katika Nyanja ya elimu kwa kujenga Seminari 17 katika maeneo mbalimbali ya nchi, na vyuo viwili ya ualimu, kule Iringa na Himo, mikoa ya Kilimanjaro.

Asanteni
Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali.
KIPINDI CHA UTAMBULISHO
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali
 Rev. Ronald Swai, Sekretari Mkuu akiwakaribisha waandishi wa habari
 Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini

kushoto ni bloga wa Rumafrica For All Nations, Rulea Sanga

kulia ni bloga kutoka RUMAFRICA FOR ALL NATIONS, Rulea Sanga
 Baadhi ya waandishi wa habari, kushoto ni Silas Mbise wa  Gospel Kitaa na Wapo Redio
 Waaandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Askofu Mkuu.
 Mathew Sasali
  Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini akijitambulisha

KIPINDI CHA ASKOFU MKUU DK. BARNABAS MTOKAMBALI KULETA KILI ALICHOTAKA JAMII IJUE JUU YA SHEREHE YA MIAKA 75 YA UHAI WA KANISA LA TAG

Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa kwa umakini


Picha zimepigwa na Rumafrica For All Nations
www.rumaafrica.blogspot.com

ROSE MUHANDO KUZINDUA ALBAMU YAKE YA FACEBOOK AGOSTI 3/2014 JIJINI DAR.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu ka FACEBOOK ya mwimbaji wa muziki wa injili anayevuma, Rose Muhando utakaofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 3 /2014 jijini Dar es salaam, ambapo amesema baadhi ya mapato yatakwenda kuviwezesha mitaji zaidi ya vituo 10 vya watoto yatima jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kwa Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi huo unaoatarajiwa kuwa mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa waimbaji wa muziki wa injili.

KUTOKA BLOGU YA UNCLE JIMMY: ANGEL BENARD KUJA NA VIDEO YA I NEED YOU TO REIGN,PAMOJA NA DOCUMENTARY YA MAISHA YAKE.

Posted by Uncle Jimmy Sunday, May 18, 2014



Angel Benard kuptia wimbo wake wa I need you to reign uliomtangaza vizuri Tanzania,Kenya,Rwanda,Bostswana,America,Jamaica,na South Africa kwa mwaka huu 2014 na kujipatia mashabiki wengi….Ana mshukuru Mungu kwa hatua aliyoanza taratibu za kurekodi video ya "I need you to reign" .Angel akiongea na blog amesema kuwa
ameona kibali kikubwa hivyo watu wengi wanasubiri video yake kwa hamu kubwa.

Video ya mwimbo huu inategemewa kutoka mwishoni wa mwezi huu hivyo kwa sasa hakupenda kutaja director wa video hiyo,hivyo kama wewe shabiki wa Angel Benard kaa vizuri kwani itakua surprise kwako.

Picha mbili ni sehemu ya maandalizi ya video hiyo zilizo fanyika chini ya “Mayur Nayi” (Photo Shooter)





Lakini pia anaendelea kusema haya ni maandalizi ya Documentary ya safari yake katika Utumishi toka 2005,mambo aliyokutana nayo katika muziki,huduma,maisha hadi hapo alipo.Mdau wangu kaa tayari kwa ajili ya documentary hiyo itakayokuwa launched mwezi wa tisa.

KUTOKA SIFA ZIFUME 2011: CLOSE THAN BEFORE YALETA GUMZO JIJINI

Posted by Sifa Zifume Monday, September 19, 2011

Jioni Ya Jana pale kwenye Ukumbi wa CCC Next Level Concert ilikuwa na theme ya "Close Than Before" ambayo ilikuwa ni ya aina yake wakazi mbalimbali wa jiji la Dar-es-Salaam na Vitongoji vyake walijumuika kwa pamoja kumsifu Mungu.

Tamasha hili la Next Level ambalo huandaliwa na Kanisa la CCC hufanyika kila mwaka mara moja hapa Tanzania, na kila mwaka Next Level imekuwa ikienda kwenye Next Levels, mwaka huu ilikuwa ni Heavy Weight yaani nzito kuliko ya Mwaka Jana.

Kabla ya Next Level Team kupanda walitanguliwa watumishi mbalimbali, kati ya Waliohudumu siku ya Jana ni ni Holy Of Hollies, President Chavala, Shekhina Dancers, John Lisu na Mchungaji Masanja Mkandamizaji.


Huyu Jamaa ni wa Holy Of Hollies alikuwa akiongoza swaga za Ukweli Jana Jioni kwenye Next Level Concert





The Great John Lisu akiwa anaongoza Uimbaji katika Siku Ya Jana


Uncle Jimmy Temu Blogger kutoka www.unclejimmytemu.blogspot.com akiwa anadaka matukio ya Jana.


Blogger Rulea mwenye Kamera kutoka www.rumaafrica.blogspot.com.com akiweka sawa mitambo yake tayari kwa kazi.


Angel Benard akiongoza The Glorious Band siku Ya Jana.




Mabisa wa Glorious akiwa kazini (Picha ya Juu) Glorious Band wakiwa kazini


Bishop Ranwell Mwenisongole akiongea Jioni Ya Jana


Mc wa Event Isaack akiwa kazini.

















Picha zikionesha Next Level Praise and Worship Team

Kama kuna event Ya Gospel then ukamkosa Seth ujue hiyo Event haina Kiwango.


Kikazi zaidi.

President Chavala akifanya mambo siku ya Jana. President Chavala is a Comedian



Masanja Mkandamizaji akikandamiza siku ya Jana katika Next Level.




Shekhina Dancers wakifanya kweli Jana Jioni.

Wadau

Chama Langu la Ukweli la Kutifua Tifua