HEADER

HEADER

Thursday, June 26, 2014

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KUUNGANA NA KANISA LA TAG KUSHEREKEA MIAKA 75 YA UHAI MKOANI MBEYA -ASKOFU MKUU WA TAG DKT. BARNABAS MTOKAMBALI

Rumafrica ilifika katika Makao Makuu ya Kanisa la TAG Ubungo hapa jinni Dar es Salaam na iliweza kuhudhuria kikao kilichoandaliwa na Askofu Mkuu Dk. Barnabas Mtokambali  ambapo aliweza kutueleza juu ya sherehe ya miaka 75 ya uhai wa kanisa la TAG itakayofanyia mkoani Mbeya katika viwanja vya Sokoine siku ya tarehe 13/07/2014. Mkutano huu ulihudhuriwa na waandishi wa habari mbalimbali.  Askofu Mkuu Dk. Barnabas alikuwa na haya ya kusema:
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali
Ninawasalimu nyote katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, karibuni hapa TAG Makao Makuu.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) linasherekea miaka 75 ya uhai  wake hapa nchini, tangu lilipoanzishwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu mwaka 1939. Kwa kuzingatia umuhimu wa maadhimisho hayo, Mkutano Mkuu wa TAG, (chombo cha kimaamuzi) katika kikao chake cha kwanza mwaka 2012, uliamua kutangaza mwaka 2014 kuwa ni wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 ya TAG

Kutokana na maadhimisho hayo, kanisa la liliandaa maadhimisho katika ngazi zake mbalimbali za kimaongozi, kuanzia kanisa la mahali pamoja, sehemu (section) majimbo ambayo ni sawa na mikoa ya kikanisa na ngazi ya taifa ambayo kilele chake ni Julai 13 mwaka huu, katika uwanja wa sokoine Mbeya na Raisi wa Jamhuri wa Muungano Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, atakuwa  Mgeni Rasmi.

Katika maadhimisho hayo yatakayokusanya watu zaidi ya 2,000, mjini Mbeya, pia atakuwepo mwenyekiti wa makanisa ya Assemblies of God Duniani, Dk. George Wood, Maaskofu kutoka mataifa mbalimbali kama vile; Amerika, Uingereza, Ethiopia, Zambia, Rwanda, Malawi, Msumbuji, India na wengine wengi.

Wakati huu wa kuadhmisha miaka 75 ya kanisa letu, ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa yale aliyotuwezesha kufanya kwaajili ya kuujenga Ufalme Wake na kudhihirisha upendo wetu kwa jamii kwa kushiriki katika masuala mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji mkubwa.

Wakati wa maafa kama njaa, mafuriko na majanga mengine ya kijamii kwa neema ya Mungu kanisa la TAG limejihusisha kikamilifu kusaidia kwa kugawa vyakula katika mikoa ya Dodoma na kwingine, pia limechimba visima katika maeneo yenye ukame.

Mwaka huu wa maadhimisho kanisa la TAG limekuwa na miradi mingi iliyoelekeza waumini wake katika kuchangia damu mahospitalini karibu kila wilaya nchini, wagonjwa wameongezwa damu zilizotoka kwa wenzao wa TAG wakiongozwa na viongozi wa kitaifa. Pia kanisa la TAG limepeleka misaada ya kimwili na kiroho kwa waliofungwa gerezani, vituo vya yatima na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika kilele cha maadhimisho ya kanisa letu kule Mbeya, kanisa limeamua kutoa vyandarua zaidi ya 35,000 vyenye thamani zaidi ya Tsh. 270 milion. Vyandarua hivi vitagawiwa kwa kila kitanda cha hospitali katika mikoa ya Nyanda za Juuu Kusini, mikoa ya Njome, Mbeya na Rukwa, bila kujali hospitali husika inamilikiwa na nani.

Lengo la kugwa vyandarua hivi ni kuhakikisha kuwa ugonjwa wa malaria ambao kwa miaka mingi umeongeza kwa kusababisha vifo, hasa vya watoto na wajawazito unakabiliwa ipasavyo.

Pamoja na misaada hii ya  moja kwa moja, kanisa la TAG lipo katoika mcjhakato makini wa kusaidia Watanzania katika Nyanja ya elimu kwa kujenga Seminari 17 katika maeneo mbalimbali ya nchi, na vyuo viwili ya ualimu, kule Iringa na Himo, mikoa ya Kilimanjaro.

Asanteni
Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali.
KIPINDI CHA UTAMBULISHO
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali
 Rev. Ronald Swai, Sekretari Mkuu akiwakaribisha waandishi wa habari
 Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini

kushoto ni bloga wa Rumafrica For All Nations, Rulea Sanga

kulia ni bloga kutoka RUMAFRICA FOR ALL NATIONS, Rulea Sanga
 Baadhi ya waandishi wa habari, kushoto ni Silas Mbise wa  Gospel Kitaa na Wapo Redio
 Waaandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Askofu Mkuu.
 Mathew Sasali
  Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini akijitambulisha

KIPINDI CHA ASKOFU MKUU DK. BARNABAS MTOKAMBALI KULETA KILI ALICHOTAKA JAMII IJUE JUU YA SHEREHE YA MIAKA 75 YA UHAI WA KANISA LA TAG

Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa kwa umakini


Picha zimepigwa na Rumafrica For All Nations
www.rumaafrica.blogspot.com

No comments:

Post a Comment