HEADER

HEADER

Thursday, June 26, 2014

KUTOKA BLOGU YA SAMSASALI: PURE EXTRAVAGANZA KUANZA KUONEKNA AGAPE TELEVISION

Posted by Samuel Sasali on Thursday, June 14, 2012

Blog Ilipofanya Mahojiano na Waandaaji wa Kipindi, Kushoto ni Uncle Jimmy, Papaa Ze Blogger akishusha Maswali, Kulia ni Angel Benard na Fred.

Pure Extravaganza ni Kipindi Kipya Cha Tv kitakachokuwa kikirushwa katika Kituo Cha Agape Television, almaarufu ATN.


Kipindi hicho kitakachokuwa na mchanganyiko wa hard talks, music, Elimu, Mapishi na Afya kitaanza kurushwa kila siku ya Jumanne kuanzia saa 1:30 Jioni.


Blog iliteta na Waandaaji na Watangazaji wa Kipindi hicho ambao ni Fred Msungu pamoja na Mwanamuziki Angel Benard walisema wamekuja kivingine katika kuleta radha mpya ya Vipindi Vya Television za Kikristo.

Fred Msungu akifanya Kipindi Cha Radio.

Fred Msungu ambaye amefanya kazi katika Radio ya Ushindi Mkoani Morogoro, lakini pia Mwanamuziki ambaye amekuwa Mstari Wa Mbele katika Events kubwa za Jijini, kama Aflewo, Campus Night na FoF amesema amekuja na mawazo Mbadala katika kuendesha vipindi Vya Tv. Kwa sasa Fred Msungu anafanya kazi na Pure Ministry inayofanya kazi kwenye Vyuo na Shule za hapa Tanzania.

Angel Bernard Ndani Ya Pozz

Angela Bernard ambaye ni Mwanafunzi anayemalizia masomo yake pale Mlimani, pia ni Kiongozi wa Glorious Band lakini ni mmoja wa Founders wa Pure Ministry hapa Tanzani. Akiongea na Blog amesema Amejipanga ki sawa sawa.

Watangazaji hawa wamesema Tazama ATN kila Jumanne, kisha Utaona Radha Tofauti kwenye Runinga yako.

Baada Ya Interview Tukapata Picha Ya Pamoja

No comments:

Post a Comment