HEADER
Wednesday, August 13, 2014
RUMAFRICA ILIVYO WEZA KUSEMA MACHACHE JUU YA UJIO WA VIDEO YA ANGEL BENARD YA "NEED YOU TO REIGN" NCHINI KENYA
Mwanadada
Angel Benard sasa amekuja kivingine kabisa kuanzia uimbaji hadi video
zake. Mungu anazidi kumuonyesha njia iliyo sahihi katika kazi yake ya
kumtuminkia. Angel mara nyingi amekuwa akilia sana na waimbaji wenzake
kuwa wanatakiwa kufanya vitu vikali vya kumtukuza Mungu. Tumebweteka
sana katika kazi ya Mungu, tunaichukulia simple sana, waswahili wanasema
"Bora liende" Tunatakiwa kuwa na hamu ya kufanya vizuri kwa utukufu wa
Mungu.
Angel Beanrd akiwa location
Leo hii mdada wa Yesu amekuja kuonyesha mfano na changamoto kwa waimbaji wengine kutafuta watu wenye kiwango katika v0ideo zao ili ziwe na viwango vya kimataifa na ikiwezekana kazi za walokole ziwe mfano mkubwa kwa watu wa mataifa. Tukumbuke tunamtumikia Mungu ambaye ni tajiri sana, lakini kazi zetu zinaonekana zimechoka sana. Tuache kupenda vitu vya bei chini bali tuangalie thamani ya huyu tunayemtumikia
Angel Benard ambaye mara nyingi huonekana akiwa na furaha na amani anapofanya kazi ya Mungu, kama unavyomuona
Hongera sana Angel Benard kwa hatu uliyofikia mpaka ukaamua kuvuka boda mpaka nchini Kenya kufanya kazi na watu wenye uwezo mkubwa. Hujaogopa mapesa meni bali umeangalia kile Mungu ameweka ndani yako. Mungu atafanya jambo kwa kupitia nyimbo zako hizi kali ambazo hazibagui ni mtuwa dini gani wa kusikiliza.
Angel Beanrd akitafakari jambo katika zoezi la kuandaa video yake
Angel Benard akiongea na Rumafrica kwa njia ya Watsap amesema kazi yake ya kideo hiki inafanywa na director Kevin Bosco na imefanyiwa katika mazingira ya Old Stonange Paradise Nairobi Kenya na wimbo ni "Need you to reign"
SIKILIZA NYIMBO MPYA AMBAZO ZINAFANYIWA SHOOTING HIVI KARIBUNI ZA ANGEL BENARD. SUBTITLE IMEFANYWA NA RUMAFRICA
Monday, June 30, 2014
MAPICHA: MUNGU NI MWEMA KWANGU DAIMA
Ninalindwa, ninatunzwa, ninalishwa, ninavishwa na huyu mpenzi wa roho
yangu YESU KRISTO. Sitomwacha kamwe na ninamuomba asiniache kamwe maisha
mwangu. Yesu amekuwa mfariji wangu ninapopitia magumu, hakika ni faraja
yangu.
Mungu amenipa kazi ya kumimbia, nami ninafanya kama alivyoniambia.Yesu Kristo hunipa kicheko kila kuitwapo leo
Ninaringa kwasababu ninaye Yesu Kristo, naye ananipenda sana...
Upendo na marafiki zangu ni moja ya amri ya Yesu Kristo ambayo ninajitahihidi kutekeleza
Unaonaje ukimpenda huyu Yesu Kristo maisha mwako
Najua unapitia magumu lakini yupo mwokozi wa hayo yote ambaye ni Bwana Yesu Kristo. Mkubali sasa
Thursday, June 26, 2014
MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI WAAGWA JIJINI DAR LEO
SISTA Cresensia Kapuli aliyepigwa risasi Jumatatu Juni 23, 2014
maeneo ya Ubungo, River Side na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
hatimaye ameagwa katika Parokia ya Makoka, Kibangu jijini Dar.
Mwili wa marehemu umeagwa na umati wa watu wa rika zote wakiwemo viongozi wa dini na serikali. Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Juni 28, 2014. Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
Masista wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Sista Cresensia Kapuli aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Juni 23, 2014.
Sista Brigitte Mbaga aliyekuwa na marehemu Cresensia Kapuli eneo la tukio siku alipopigwa risasi akiwa na simanzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond H. Mushi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick.
Mwakilishi wa mama watawa wakuu wa shirika la malkia kutoka Mbeya akilia kwa uchungu.
Jeneza likiwekwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Mbeya kwa maziko.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KUUNGANA NA KANISA LA TAG KUSHEREKEA MIAKA 75 YA UHAI MKOANI MBEYA -ASKOFU MKUU WA TAG DKT. BARNABAS MTOKAMBALI
Rumafrica ilifika katika Makao Makuu ya Kanisa la TAG Ubungo hapa jinni Dar es
Salaam na iliweza kuhudhuria kikao kilichoandaliwa na Askofu Mkuu Dk. Barnabas
Mtokambali ambapo aliweza
kutueleza juu
ya sherehe ya miaka 75 ya uhai wa kanisa la TAG itakayofanyia mkoani
Mbeya katika viwanja vya Sokoine siku ya tarehe 13/07/2014. Mkutano huu
ulihudhuriwa na
waandishi wa habari mbalimbali. Askofu
Mkuu Dk. Barnabas alikuwa na haya ya kusema:
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas
Mtokambali
Ninawasalimu nyote katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, karibuni
hapa TAG Makao Makuu.
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) linasherekea miaka 75 ya uhai wake hapa nchini, tangu lilipoanzishwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu mwaka 1939. Kwa kuzingatia umuhimu wa maadhimisho hayo, Mkutano Mkuu wa TAG, (chombo cha kimaamuzi) katika kikao chake cha kwanza mwaka 2012, uliamua kutangaza mwaka 2014 kuwa ni wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 ya TAG
Kutokana na maadhimisho hayo, kanisa la liliandaa maadhimisho katika ngazi zake mbalimbali za kimaongozi, kuanzia kanisa la mahali pamoja, sehemu (section) majimbo ambayo ni sawa na mikoa ya kikanisa na ngazi ya taifa ambayo kilele chake ni Julai 13 mwaka huu, katika uwanja wa sokoine Mbeya na Raisi wa Jamhuri wa Muungano Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, atakuwa Mgeni Rasmi.
Katika maadhimisho hayo yatakayokusanya watu zaidi ya 2,000, mjini Mbeya, pia atakuwepo mwenyekiti wa makanisa ya Assemblies of God Duniani, Dk. George Wood, Maaskofu kutoka mataifa mbalimbali kama vile; Amerika, Uingereza, Ethiopia, Zambia, Rwanda, Malawi, Msumbuji, India na wengine wengi.
Wakati huu wa kuadhmisha miaka 75 ya kanisa letu, ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa yale aliyotuwezesha kufanya kwaajili ya kuujenga Ufalme Wake na kudhihirisha upendo wetu kwa jamii kwa kushiriki katika masuala mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji mkubwa.
Wakati wa maafa kama njaa, mafuriko na majanga mengine ya kijamii kwa neema ya Mungu kanisa la TAG limejihusisha kikamilifu kusaidia kwa kugawa vyakula katika mikoa ya Dodoma na kwingine, pia limechimba visima katika maeneo yenye ukame.
Mwaka huu wa maadhimisho kanisa la TAG limekuwa na miradi mingi iliyoelekeza waumini wake katika kuchangia damu mahospitalini karibu kila wilaya nchini, wagonjwa wameongezwa damu zilizotoka kwa wenzao wa TAG wakiongozwa na viongozi wa kitaifa. Pia kanisa la TAG limepeleka misaada ya kimwili na kiroho kwa waliofungwa gerezani, vituo vya yatima na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika kilele cha maadhimisho ya kanisa letu kule Mbeya, kanisa limeamua kutoa vyandarua zaidi ya 35,000 vyenye thamani zaidi ya Tsh. 270 milion. Vyandarua hivi vitagawiwa kwa kila kitanda cha hospitali katika mikoa ya Nyanda za Juuu Kusini, mikoa ya Njome, Mbeya na Rukwa, bila kujali hospitali husika inamilikiwa na nani.
Lengo la kugwa vyandarua hivi ni kuhakikisha kuwa ugonjwa wa malaria ambao kwa miaka mingi umeongeza kwa kusababisha vifo, hasa vya watoto na wajawazito unakabiliwa ipasavyo.
Pamoja na misaada hii ya moja kwa moja, kanisa la TAG lipo katoika mcjhakato makini wa kusaidia Watanzania katika Nyanja ya elimu kwa kujenga Seminari 17 katika maeneo mbalimbali ya nchi, na vyuo viwili ya ualimu, kule Iringa na Himo, mikoa ya Kilimanjaro.
Asanteni
Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali.

KIPINDI CHA UTAMBULISHO
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas
Mtokambali
Rev. Ronald Swai, Sekretari Mkuu akiwakaribisha waandishi wa habari
Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini
kushoto ni bloga wa Rumafrica For All Nations, Rulea Sanga
kulia ni bloga kutoka RUMAFRICA FOR ALL NATIONS, Rulea Sanga

Baadhi ya waandishi wa habari, kushoto ni Silas Mbise wa Gospel Kitaa na Wapo Redio
Waaandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Askofu Mkuu.
Mathew Sasali
Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini akijitambulisha
KIPINDI CHA ASKOFU MKUU DK. BARNABAS MTOKAMBALI KULETA KILI ALICHOTAKA JAMII IJUE JUU YA SHEREHE YA MIAKA 75 YA UHAI WA KANISA LA TAG
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa kwa umakini
ROSE MUHANDO KUZINDUA ALBAMU YAKE YA FACEBOOK AGOSTI 3/2014 JIJINI DAR.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu ka FACEBOOK ya mwimbaji wa muziki wa injili anayevuma, Rose Muhando utakaofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 3 /2014 jijini Dar es salaam, ambapo amesema baadhi ya mapato yatakwenda kuviwezesha mitaji zaidi ya vituo 10 vya watoto yatima jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kwa Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi huo unaoatarajiwa kuwa mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa waimbaji wa muziki wa injili.
KUTOKA BLOGU YA UNCLE JIMMY: ANGEL BENARD KUJA NA VIDEO YA I NEED YOU TO REIGN,PAMOJA NA DOCUMENTARY YA MAISHA YAKE.
Posted by Uncle Jimmy Sunday, May 18, 2014
Angel Benard kuptia wimbo wake wa I need you to reign uliomtangaza vizuri Tanzania,Kenya,Rwanda,Bostswana,America,Jamaica,na South Africa kwa mwaka huu 2014 na kujipatia mashabiki wengi….Ana mshukuru Mungu kwa hatua aliyoanza taratibu za kurekodi video ya "I need you to reign" .Angel akiongea na blog amesema kuwa
ameona kibali kikubwa hivyo watu wengi wanasubiri video yake kwa hamu kubwa.
Video ya mwimbo huu inategemewa kutoka mwishoni wa mwezi huu hivyo kwa sasa hakupenda kutaja director wa video hiyo,hivyo kama wewe shabiki wa Angel Benard kaa vizuri kwani itakua surprise kwako.
Picha mbili ni sehemu ya maandalizi ya video hiyo zilizo fanyika chini ya “Mayur Nayi” (Photo Shooter)
Lakini pia anaendelea kusema haya ni maandalizi ya Documentary ya safari yake katika Utumishi toka 2005,mambo aliyokutana nayo katika muziki,huduma,maisha hadi hapo alipo.Mdau wangu kaa tayari kwa ajili ya documentary hiyo itakayokuwa launched mwezi wa tisa.

Subscribe to:
Posts (Atom)