Rumafrica ilifika katika Makao Makuu ya Kanisa la TAG Ubungo hapa jinni Dar es
Salaam na iliweza kuhudhuria kikao kilichoandaliwa na Askofu Mkuu Dk. Barnabas
Mtokambali ambapo aliweza
kutueleza juu
ya sherehe ya miaka 75 ya uhai wa kanisa la TAG itakayofanyia mkoani
Mbeya katika viwanja vya Sokoine siku ya tarehe 13/07/2014. Mkutano huu
ulihudhuriwa na
waandishi wa habari mbalimbali. Askofu
Mkuu Dk. Barnabas alikuwa na haya ya kusema:
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas
Mtokambali
Ninawasalimu nyote katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, karibuni
hapa TAG Makao Makuu.
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) linasherekea miaka 75 ya uhai wake hapa nchini, tangu lilipoanzishwa kwa
uongozi wa Roho Mtakatifu mwaka 1939. Kwa kuzingatia umuhimu wa maadhimisho
hayo, Mkutano Mkuu wa TAG, (chombo cha kimaamuzi) katika kikao chake cha kwanza
mwaka 2012, uliamua kutangaza mwaka 2014 kuwa ni wa maadhimisho ya Jubilei ya
miaka 75 ya TAG
Kutokana na maadhimisho hayo, kanisa la liliandaa maadhimisho katika ngazi zake
mbalimbali za kimaongozi, kuanzia kanisa la mahali pamoja, sehemu (section)
majimbo ambayo ni sawa na mikoa ya kikanisa na ngazi ya taifa ambayo kilele
chake ni Julai 13 mwaka huu, katika uwanja wa sokoine Mbeya na Raisi wa Jamhuri
wa Muungano Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, atakuwa Mgeni Rasmi.
Katika maadhimisho hayo yatakayokusanya watu zaidi ya 2,000, mjini Mbeya, pia
atakuwepo mwenyekiti wa makanisa ya Assemblies of God Duniani, Dk. George Wood,
Maaskofu kutoka mataifa mbalimbali kama vile; Amerika, Uingereza, Ethiopia,
Zambia, Rwanda, Malawi, Msumbuji, India na wengine wengi.
Wakati huu wa kuadhmisha miaka 75 ya kanisa letu, ni wakati wa kumshukuru Mungu
kwa yale aliyotuwezesha kufanya kwaajili ya kuujenga Ufalme Wake na
kudhihirisha upendo wetu kwa jamii kwa kushiriki katika masuala mbalimbali kwa
jamii yenye uhitaji mkubwa.
Wakati wa maafa kama njaa, mafuriko na majanga mengine ya kijamii kwa neema ya
Mungu kanisa la TAG limejihusisha kikamilifu kusaidia kwa kugawa vyakula katika
mikoa ya Dodoma na kwingine, pia limechimba visima katika maeneo yenye ukame.
Mwaka huu wa maadhimisho kanisa la TAG limekuwa na miradi mingi iliyoelekeza
waumini wake katika kuchangia damu mahospitalini karibu kila wilaya nchini,
wagonjwa wameongezwa damu zilizotoka kwa wenzao wa TAG wakiongozwa na viongozi
wa kitaifa. Pia kanisa la TAG limepeleka misaada ya kimwili na kiroho kwa
waliofungwa gerezani, vituo vya yatima na kufanya usafi katika maeneo
mbalimbali nchini.
Katika kilele cha maadhimisho ya kanisa letu kule Mbeya, kanisa limeamua kutoa
vyandarua zaidi ya 35,000 vyenye thamani zaidi ya Tsh. 270 milion. Vyandarua
hivi vitagawiwa kwa kila kitanda cha hospitali katika mikoa ya Nyanda za Juuu
Kusini, mikoa ya Njome, Mbeya na Rukwa, bila kujali hospitali husika
inamilikiwa na nani.
Lengo la kugwa vyandarua hivi ni kuhakikisha kuwa ugonjwa wa malaria ambao kwa
miaka mingi umeongeza kwa kusababisha vifo, hasa vya watoto na wajawazito
unakabiliwa ipasavyo.
Pamoja na misaada hii ya moja kwa moja,
kanisa la TAG lipo katoika mcjhakato makini wa kusaidia Watanzania katika Nyanja
ya elimu kwa kujenga Seminari 17 katika maeneo mbalimbali ya nchi, na vyuo
viwili ya ualimu, kule Iringa na Himo, mikoa ya Kilimanjaro.
Asanteni
Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali.
KIPINDI CHA UTAMBULISHO
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas
Mtokambali
Rev. Ronald Swai, Sekretari Mkuu akiwakaribisha waandishi wa habari
Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini
kushoto ni bloga wa Rumafrica For All Nations, Rulea Sanga
kulia ni bloga kutoka RUMAFRICA FOR ALL NATIONS, Rulea Sanga
Baadhi ya waandishi wa habari, kushoto ni Silas Mbise wa Gospel Kitaa na Wapo Redio
Waaandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Askofu Mkuu.
Mathew Sasali
Kulia ni Askofu Mkuu Geoffrey Massawe wa Jimbo la Mashariki Kaskazini akijitambulisha
KIPINDI CHA ASKOFU MKUU DK. BARNABAS MTOKAMBALI KULETA KILI ALICHOTAKA
JAMII IJUE JUU YA SHEREHE YA MIAKA 75 YA UHAI WA KANISA LA TAG
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dk. Barnabas
Mtokambali
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa kwa umakini